Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Hii hapa fursa kusoma AI, sayansi ya data bure Japan

Дата публикации: 12-08-2026 09:22:46

Wanafunzi Watanzania wanaotamani kujikita katika teknolojia za kisasa wamepata fursa ya kusoma bila malipo sayansi ya data na Akili Unde (AI) katika Chuo Kikuu cha Tokyo, Japan, kwa miezi mitatu bure.

Основное содержимое страницы с новостью.

Dar es Salaam. Wanafunzi Watanzania wanaotamani kujikita katika teknolojia za kisasa wamepata fursa ya kusoma bila malipo sayansi ya data na Akili Unde (AI) katika Chuo Kikuu cha Tokyo, Japan, kwa miezi mitatu bure.

Fursa hiyo imetangazwa leo Jumatano, Agosti 12, 2026 na Ubalozi wa Tanzania nchini Japan,  ukiwaalika wanafunzi kuomba nafasi ya mafunzo hayo yatakayotolewa kupitia Maabara ya Matsuo-Iwasawa ya Chuo Kikuu cha Tokyo.

Kwa mujibu wa tangazo hilo la ubalozi, mafunzo hayo yataanza Septemba 17 hadi Desemba 17, 2026, yakilenga kuwajengea washiriki ujuzi unaohitajika katika teknolojia zinazotajwa kuwa na nafasi kubwa katika uchumi na soko la ajira la sasa na baadaye.

Kupitia tangazo hilo ubalozi umewataka wanafunzi wenye sifa nchini Tanzania kutumia fursa hiyo kuongeza ujuzi wao katika maeneo ya sayansi ya data na AI, ambayo yanaendelea kuwa muhimu katika maendeleo ya teknolojia na biashara duniani.

Miongoni mwa mada zitakazofundishwa ni sayansi ya data, ujifunzaji wa mashine, uchakataji na uwasilishaji wa data pamoja na matumizi ya sayansi ya data katika biashara.

Fursa hiyo inawalenga wanafunzi kuanzia ngazi ya sekondari hadi shahada ya uzamivu, huku waombaji wakitakiwa kuwa wanaosoma katika taasisi za elimu inayotambuliwa.

Aidha, mwombaji anatakiwa kuwa mwanafunzi wakati wa kuanza kwa programu hiyo, awe na uwezo wa kujifunza kwa kujitegemea na kuwa tayari kushiriki kikamilifu katika mafunzo na kukamilisha mahitaji yake.

Kwa Tanzania, fursa hiyo inaweza kuwa sehemu ya kuongeza idadi ya vijana wenye ujuzi katika maeneo ya teknolojia yanayokua kwa kasi, hasa katika kipindi ambacho matumizi ya AI na uchanganuzi wa data yanaingia katika sekta mbalimbali za uchumi.

Tangazo hilo limewataka wanafunzi wanaotaka kuomba kuwasilisha maombi yao kupitia mfumo wa Omnicampus, huku wakitakiwa kuwa na anuani ya barua pepe inayotumika.

“Baada ya usajili na kuidhinishwa, waombaji watapata taarifa za kuingia kwenye mfumo wa Omnicampus na kuendelea na hatua za maombi. Katika mfumo huo, mwombaji anatakiwa kuchagua kozi yenye jina “GCI World 2026 September” na kukamilisha maombi,” imeeleza taarifa hiyo.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Accordo Ue-Giappone su intelligenza artificiale e dati per servizi “senza barriere”09.0705-05-2026
2Τελευταία εβδομάδα για αιτήσεις στο πρόγραμμα υποτροφιών AKTOR4TheFuture 0515-06-2026
3EAC yageukia AI kukabili Ebola09.7812-08-2026
4Tusiache kuwalea hata kama wako vyuoni0530-06-2026
5Hivi ndivyo mwanachuo anaweza kujiajiri01012-08-2026
6Ongezeko la wahitimu wa vyuo, wadau watoa pendekezo01010-08-2026
7Осенью в 100 вузах России стартуют программы обучения технологиям ИИ0022-07-2019
8Фан-та-сти-ка🔊 Запускаем Всероссийскую олимпиаду по искусственному интеллекту и раскрываем тему ...5703-07-2026
9МТС, МФТИ и СКОЛКОВО набирают студентов в магистратуру "Цифровые технологии в бизнесе"0002-07-2021
10Искусственный интеллект поможет в поиске работы выпускникам томского вуза0023-11-2020

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 5.72. Источник: www.mwananchi.co.tz.