Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Ongezeko la wahitimu wa vyuo, wadau watoa pendekezo

Дата публикации: 10-08-2026 13:52:47

Soma zaidi hapa...

Основное содержимое страницы с новостью.

Prime

Jumatatu, Agosti 10, 2026

By  Aurea Simtowe

Mwandishi wa Habari

Mwananchi

Muktasari:
  • Takwimu za Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) zinaonesha kuwa, idadi ya wahitimu wa ngazi zote imeongezeka kutoka 48,621 mwaka 2020 hadi 66,414, huku wale wa shahada ya kwanza wakibeba asilimia 70.6 ya wahitimu wote.

Dar es Salaam. Idadi ya vijana wanaohitimu vyuo vikuu imeongezeka kwa asilimia 36.5 kati ya mwaka 2020 hadi 2025, wadau wametaka kasi hiyo iende sambamba na kuboresha fursa zinazoajiri watu wengi.

Takwimu za Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) zinaonesha kuwa, idadi ya wahitimu wa ngazi zote imeongezeka kutoka 48,621 mwaka 2020 hadi 66,414, huku wale wa shahada ya kwanza wakibeba asilimia 70.6 ya wahitimu wote.

Mbali na wahitimu wa shahada ya kwanza kuongezeka, fani ya elimu katika kipindi husika ndiyo iliyokuwa ikitoa wahitimu wengi zaidi kuliko fani nyingine yoyote.

Fani hiyo inatoa wahitimu wengi, licha ya takwimu za TCU kuitaja kuwa miongoni mwa zile zinazopoteza mvuto kwa wanafunzi baada ya kushushwa kutoka namba moja kati ya zile zilizokuwa zikidahili wanafunzi wengi, ikipishwa na biashara.

TCU inaonesha kuwa katika kipindi husika, fani ya elimu ilizalisha wahitimu 74,831, ambapo katika mwaka 2021 walikuwa 14,050, mwaka 2022 (15,335), mwaka 2023 (15,103), mwaka 2024 walikuwa 13,834 na mwaka 2025 walikuwa 16,509.

Nini maana yake

Akizungumzia suala hilo, mchambuzi wa uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki Ruaha (Rucu), Dk Isdori Minani amesema wakati nchi ikishuhudia ongezeko la wahitimu, kuna haja ya kuongeza nguvu katika kubadili mtazamo na kuwaandaa wahitimu kujiajiri na kutengeneza fursa, badala ya kusubiri kuajiriwa.

“Hii itamjenga mtu akiwa mwaka wa pili au tatu, anajua kabisa nikitoka hapa nafanya kitu fulani, si mtu awe anaangalia aajiriwe tu. Ukimuuliza hana chochote kichwani kwa sababu elimu aliyopata haikumsaidia na inabidi pia kuangalia namna tunavyofundisha wanafunzi wetu,” amesema.

Ameshauri kuwa, ili hilo lifanikiwe haraka, ni vyema vyuo vikuu kuimarisha uhusiano na soko la ajira ili kuhakikisha programu zinazotolewa zinawaandaa wanafunzi wenye ujuzi unaohitajika na waajiri.

Amesema vyuo vinapaswa kuwashirikisha wataalamu waliopo katika sekta mbalimbali katika ufundishaji wa baadhi ya masomo, ili wanafunzi wapate uelewa wa moja kwa moja kuhusu mahitaji halisi ya soko la ajira.

“Hatua hii itasaidia kupunguza pengo kati ya kile kinachofundishwa vyuoni na kile kinachohitajika katika maeneo ya kazi, huku ikiwapa wahitimu uwezo wa kuajiriwa au kujiajiri baada ya kumaliza masomo,” amesema.

Amesema kwa sasa kuna sababu mbalimbali zinazofanya wahitimu wengi kushindwa kuendana na mahitaji ya soko la ajira, ikiwamo ukosefu wa ujuzi laini (soft skills) na changamoto za tabia.

Amesema mhitimu anaweza kuwa na maarifa ya kutosha kitaaluma, lakini akakosa tabia na mwenendo unaohitajika katika mazingira ya kazi, hali inayoweza kumfanya mwajiri asimwajiri.

“Unaweza kuwa unafahamu kitu kichwani, lakini tabia ikawa changamoto. Inakuwa ngumu mtu kukuajiri. Watu wanaenda kwenye maofisi kufanya masomo kwa vitendo, lakini mwisho wa siku tunapata malalamiko ya tabia hii inafanya hata ndugu wakitaka kukuweka kwenye kazi wanashindwa kwa sababu hawaoni uaminifu,” amesema.

Amesema changamoto nyingine ni namna ambavyo baadhi ya taasisi za elimu zinavyopima mafanikio ya wanafunzi, ambapo wakati mwingine msisitizo unawekwa kwenye idadi ya wanaofaulu badala ya kiwango cha uelewa na uwezo wa kutumia maarifa hayo katika mazingira halisi.

“Mara nyingi vyuoni kuna kukariri, lakini si ule uelewa. Unaweza kuona vyuo vinaangalia sana idadi ya wanaofaulu bila kujali ufaulu huo uko katika kiwango gani kinachokidhi mahitaji ya soko,” amesema.

Amesema si lazima kila mwanafunzi amalize masomo kwa ufaulu, akisisitiza kuwa kuna baadhi wanaoweza kushindwa kwa sababu hawana uwezo unaohitajika, lakini mfumo unapowalazimisha kufaulu huenda wakaingia katika soko la ajira bila kuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

“Si lazima amalize. Wengine wanaweza kushindwa, lakini wengine tunawalazimisha watu wafaulu wakati uwezo hawana. Akifika kwenye soko la ajira hawezi kufanya kazi inavyotakiwa, wakati kiukweli hakutakiwa kuwa amefaulu,” amesema.

Haya yanabainishwa wakati ambao Serikali katika mwaka 2025/2026 ilijivunia kutengeneza fursa za ajira 625,273 zilizalishwa hadi Februari 2026, kwa mujibu wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge 2026/2027.

Kati ya ajira zilizozalishwa, ajira 242,656 za wazawa zilitokana na vibali 12,549 vilivyotolewa kwa wageni, sawa na uwiano wa mgeni mmoja kwa wazawa 19, ikilinganishwa na uwiano wa mgeni mmoja kwa wazawa 10, kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni, Sura 436.

Mhitimu

Haya yanaelezwa wakati tayari baadhi ya wahitimu wameamua kutumia fursa walizonazo kwa ajili ya kujenga maisha yao, ikiwemo kujiajiri na baadhi kuendeleza yale waliyokuwa wanayafanya chuoni.

“Tangu nikiwa niko chuo nilikuwa nauza nguo za mitumba kwa wanafunzi wenzangu, hivyo nilipomaliza nimeamua kuweka nguvu zote huko. Hadi sasa bado sijapata sehemu maalumu ya kufanyia, lakini nimeongeza nguvu kujitangaza kwenye mitandao ya kijamii,” amesema Batuli Mussa, mhitimu wa shahada ya bima.

Amesema jambo hilo limemfanya kutotetereka na badala yake kuangalia vitu alivyokuwa hawezi kuvifanya.

Nini kifanyike

Akizungumzia suala hilo, Mchambuzi wa Uchumi, Massawe Assey, amesema kinachopaswa kupewa kipaumbele si kuongeza idadi ya wahitimu pekee, bali kuhakikisha elimu inayotolewa inaendana na mahitaji ya uchumi na soko la ajira.

“Serikali inapaswa kutumia takwimu za ajira na mahitaji ya wataalamu katika sekta mbalimbali kupanga udahili wa vyuo, huku ikihamasisha zaidi fani zenye mahitaji makubwa,” amesema.

Amesema pia vyuo vinapaswa kushirikiana kwa karibu na sekta binafsi katika kuandaa mitaala na kutoa mafunzo kwa vitendo ili wahitimu wawe na ujuzi unaohitajika kazini.

Pia, Serikali inapaswa kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara ili kuchochea shughuli za kiuchumi na kuongeza fursa za ajira kwa idadi inayoongezeka ya vijana wanaoingia katika soko la ajira.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Hivi ndivyo mwanachuo anaweza kujiajiri01012-08-2026
2Wahadhiri vyuo vikuu watoa tamko kupinga kamatakamata0520-07-2026
3Hii hapa mianya maandalizi ya walimu tarajali0030-06-2026
4Ijue siri ya kisukari iliyojificha kwenye wali, ugali01007-08-2026
5Tamu, chungu kupigana busu kiafya0002-07-2026
6Hii hapa sababu kukosa usingizi ukiwa na uchovu08.107-08-2026
7Mbinu kukabili msongo wa mawazo kwenye familia0506-07-2026
8Yanayowasubiri wahitimu mitaani0020-07-2026
9Ulaji, mazoezi silaha magonjwa yasiyoambukiza01007-08-2026
10Migogoro inapogeuka rafiki wa ndoa01009-08-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 10. Источник: www.mwananchi.co.tz.