Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), imeanzisha mpango wa kutumia Akili Unde (AI) kukabiliana na milipuko ya Ebola, huku zaidi ya vijana 20,000 wakitarajiwa kushiriki katika kutafuta suluhisho za kiteknolojia.
Jumatano, Agosti 12, 2026
Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia Sekta za Miundombinu, Uzalishaji, Kijamii na Kisiasa, Aguer Ariik Malueth, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa kutumia Akili Unde (AI) kukabiliana na milipuko ya Ebolajijini Arusha.
Arusha. Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), imeanzisha mpango wa kutumia Akili Unde (AI) kukabiliana na milipuko ya Ebola, huku zaidi ya vijana 20,000 wakitarajiwa kushiriki katika kutafuta suluhisho za kiteknolojia.
Mpango huo umezinduliwa leo Jumatano, Agosti 12, 2026 na Sekretarieti ya EAC kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani kupitia EAC AI Alliance, ukilenga vijana wabunifu, watafiti na wanafunzi kuandaa mifumo ya AI itakayosaidia kugundua milipuko ya Ebola, kujiandaa na kutoa mwitikio wa haraka.
Hatua hiyo imekuja wakati milipuko ya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Uganda ikiendelea kuibua wasiwasi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Arusha, Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia Miundombinu, Sekta za Uzalishaji, Kijamii na Kisiasa, Aguer Ariik Malueth amesema mpango huo utawapa wananchi wa Afrika Mashariki ujuzi wa kutumia AI kutatua changamoto za kikanda.
“Lengo letu ni kuhakikisha wananchi wa Afrika Mashariki wanapata ujuzi, maarifa na ushirikiano wa kutumia AI kutatua changamoto, kutengeneza ajira, kuboresha huduma za umma na kuandaa suluhisho kwa changamoto za ukanda wetu,” amesema.
Amesema EAC AI Alliance inalenga kujenga mfumo wa kikanda wa ubunifu utakaowezesha Afrika Mashariki kushindana katika uchumi wa kidijitali duniani.
Katika mpango huo, washiriki watashindana kuandaa suluhisho za kidijitali kwa changamoto za afya na sekta nyingine, huku zawadi ya jumla ikiwa Dola 50,000 za Marekani, sawa na takribani Sh130 milioni.
Miongoni mwa changamoto hizo ni Ebola, ambapo washiriki wanatakiwa kuunda mifumo ya AI itakayosaidia katika utambuzi wa magonjwa, maandalizi na mwitikio dhidi ya milipuko.
Kwa mujibu wa EAC, mpango huo ni sehemu ya awamu ya pili ya Shindano la Ubunifu la Akili Unde ya EAC (A14EAC), linalolenga kuwapa vijana, watafiti na wajasiriamali ujuzi wa AI na kuwawezesha kutumia teknolojia hiyo kutatua changamoto za ukanda.
Mpango huo unalenga kuwafikia wananchi 20,000 kupitia mafunzo ya AI katika nchi zote nane wanachama wa EAC.
Katika hatua nyingine, EAC AI Alliance imewapokea Equity Group Holdings na Karlsruhe Institute of Technology (KIT) kuwa washirika wapya wa kimkakati katika utafiti wa AI, ujenzi wa ujuzi wa kidijitali na ubunifu.
Mkurugenzi wa Ubunifu na Teknolojia wa Equity Group, Winnie Mangeni, amesema ushirikiano huo utawasaidia vijana kuandaa suluhisho za AI zinazoweza kutumika katika sekta ya fedha na changamoto nyingine halisi.
“Tunataka washiriki wafanyie kazi changamoto halisi, wanufaike kutokana na uzoefu na kuendeleza suluhisho zao hata baada ya mashindano,” amesema.
Mkuu wa Kitengo cha Afrika Mashariki na Kati katika Wizara ya Shirikisho ya Ujerumani ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (BMZ), Joachim Schmitt, amesema msaada wa Ujerumani unatokana na umuhimu wa kuwa na mkakati wa pamoja wa kikanda katika maendeleo ya AI.
Amesema Afrika imevutia uwekezaji wa Dola 1.25 bilioni katika AI tangu 2019, lakini asilimia 80 ya uwekezaji huo umeelekezwa katika nchi nne pekee.
Amesema Afrika pia ina chini ya asilimia moja ya uwezo wa vituo vya kuhifadhi na kuchakata data duniani, licha ya kuwa na takribani asilimia 18 ya watu wote duniani.
Shindano la kwanza la A14EAC lililofanyika mwaka 2025, liliwashirikisha washiriki 3,891 kutoka vyuo vikuu 57 vya Burundi, DRC, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Hii hapa fursa kusoma AI, sayansi ya data bure Japan | 0 | 5.72 | 12-08-2026 |
| 2 | Phase 3 trial of Ebola vaccine to begin within weeks in Congo | 0 | 9.99 | 11-08-2026 |
| 3 | МЧС станет участником программы "Искусственный интеллект" | 0 | 0 | 11-02-2020 |
| 4 | Искусственный интеллект поможет медикам ДНР установить диагноз пациента | 0 | 5 | 21-07-2026 |
| 5 | ИИ против вспышек вирусов: какие инфекции способны вызвать пандемию? | 5 | 7 | 08-07-2026 |
| 6 | DR Congo facing largest ever Ebola outbreak – WHO | 0 | 10.96 | 03-08-2026 |
| 7 | In Somalia, AI Is Helping Deliver Food to Hungry Families | 0 | 5.85 | 04-08-2026 |
| 8 | Oxford Bundibugyo ebolavirus vaccine candidate receives CEPI backing | 0 | 5.45 | 01-06-2026 |
| 9 | NWACC, MIT reps discuss AI curriculum | 0 | 9.25 | 24-07-2026 |
| 10 | В Ненецком АО начали тестировать искусственный интеллект для выявления опасных заболеваний | 0 | 0 | 28-08-2019 |