Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Manchester City yakutwa na hatia EPL, yasubiri kiama

Дата публикации: 25-09-2026 15:53:05

Soma hapa...

Основное содержимое страницы с новостью.

Manchester City imekutwa na hatia ya makosa 114 kati ya 115 ya uvunjaji wa kanuni za fedha za Ligi Kuu England (EPL).

Mamlaka inayosimamia Ligi Kuu England iliituhumu klabu hiyo kwa kufanya udanganyifu katika masuala ya kifedha na utawala yaliyofanyika kwa nyakati tofauti kuanzia msimu wa 2009/2010 hadi mwaka 2023.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa na jopo huru ambalo lilihitimisha usikilizaji wake mwaka 2024.

Tangu wakati huo, kumekuwa na muda mrefu wa kusubiria majibu ya uamuzi huo jambo ambalo lilianza kukatisha tamaa watu wengi ambao wana shauku ya kuona hukumu ya mashtaka hayo.

Na imefichuka kwamba tayari jopo linaloshughulikia jambo hilo limeshamaliza kazi yake na klabu zimeshajulishwa kuhusu uamuzi huo.

Kukutwa na hatia katika mashtaka hayo kunaweza kupelekea adhabu nzito kwa Manchester City ambazo zinaweza kuiathiri ushiriki wake kwenye Ligi Kuu England (EPL).

Miongoni mwa adhabu hizo ni kukatwa pointi jambo linaloweza kuifanya inyang’anywe mataji ya EPL ambayo ilitwaa katika misimu husika.

Inaripotiwa kwamba Manchester City inajipanga kukata rufaa juu ya uamuzi huo.

Msemaji wa Manchester City, amesema kwamba klabu hiyo inasubiria uamuzi wa bodi inayoshughulikia suala hilo.

“Mchakato wa Ligi Kuu unaendelea ukiwa na viashiria vya kumalizika na suala lina usiri mkubwa. Nafasi ya Manchester City inabakia kuwa ileile kama ya taarifa ya klabu ya Februari 2023,” amesema Msemaji huyo.

Mara zote, Manchester City imekuwa ikikanusha kuwa na hatia ya makosa hayo ambayo inatuhumiwa kuyafanya ndani ya miaka 14.

Awali ilishtakiwa kwa makosa 130 lakini yalipunguzwa hadi kubakia makosa 115.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Ureno yaanza kibabe Ligi ya Mataifa Ulaya01025-09-2026
2Kanuni yazigharimu Yanga, Simba mamilioni01025-09-2026
3Hii hapa sababu kukosa usingizi ukiwa na uchovu08.107-08-2026
4Shalulile apewa onyo kali Yanga01024-09-2026
5Yanayowasubiri wahitimu mitaani0020-07-2026
6Chanzo ghorofa kupigwa mnada kwa mkopo wa Sh10 milioni0520-07-2026
7Malipo posho za madaktari pasua kichwa hospitalini01020-09-2026
8Migogoro inapogeuka rafiki wa ndoa01009-08-2026
9Ulaji, mazoezi silaha magonjwa yasiyoambukiza01007-08-2026
10Manchester City found guilty of breaking Premier League’s financial fair play rules05.6425-09-2026

Классификация: Спорт. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 10. Источник: www.mwananchi.co.tz.