Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

TUONGEE KIUME: Ujumbe wenu huu hapa mnaojiita wanaume

Дата публикации: 09-08-2026 07:51:24

Kuna msemo wa wahenga ulikuwa unasema "mwanamume ni nondo," ukimaanisha ni kiumbe kigumu, kinachostahimili joto, baridi, na misukosuko yote ya maisha.

Основное содержимое страницы с новостью.

Jumapili, Agosti 09, 2026

By  Mwandishi Wetu

Mwananchi Digital

Mwananchi

Muktasari:
  • Heshima ya mwanamume ipo kwenye kifua chake cha chuma kinachobeba mizigo ya maisha, sio kwenye midomo iliyovimba kwa usongo wa mawazo.

​Dar es Salaam. Kuna msemo wa wahenga ulikuwa unasema "mwanamume ni nondo," ukimaanisha ni kiumbe kigumu, kinachostahimili joto, baridi, na misukosuko yote ya maisha.

Lakini ukitembea mitaani siku hizi, utadhani kuna kiwanda kimeanzishwa cha kutengeneza wanaume wa udongo wa mfinyanzi ambao ni wepesi kulainika, na wepesi kupasuka.

Siku hizi tumebarikiwa kupata ‘spishi’ mpya ya viumbe wanaojiita wanaume, lakini wakipishana kauli kidogo tu na wenzao, midomo inavimba utadhani wamepigwa na nyuki. Wananuna!

​Hivi karibuni kumekuwa na mtindo wa ovyo sana wa baadhi ya wanaume kuendekeza tabia ya kususa na kununa. Unakuta dume zima, lina ndevu hadi kifuani, sauti nzito kama dumu la mafuta likidondoka, lakini likiambiwa ukweli kidogo kazini au kwenye kikundi cha kahawa, linachezesha midomo, linakataa kusalimia, na kuanza kurembua macho kwa hasira.

Unajiuliza: hizi pochi za kiume (viwalo) mnavyotembea navyo mnaweka na kioo cha kujitazama usoni wakati mmenuna, au mnaweka na 'lipshine' kabisa ili midomo ikikunjana ing'ae?

Inasikitisha na kufurahisha kwa wakati mmoja kuona mwanamume ananuniana na wanaume wenzake kisa tu amejibiwa vibaya, au mawazo yake yamekataliwa kwenye kikao cha maendeleo.

Badala ya kusimama kiume, kujenga hoja, na kukabili hoja kwa hoja, yeye anachagua silaha ya kununa. Mtazame dume hilo liko kijiweni; halisemi na mtu, linatazama pembeni, na likiulizwa swali linajibu kwa kifupi "Sijui!" au linasonga mbele kwa madaha. Hivi huu si ni ulemavu wa akili na ukosefu wa kazi za kufanya?

​Mwanamume wa namna hii akirudi nyumbani nako ni majanga. Akipishana lugha kidogo na mkewe, badala ya kutatua tatizo kama kichwa cha familia, anasusa hata chakula.

Anashinda njaa huku tumbo likinguruma, anajifunika gubigubi kitandani utadhani anaumwa ndui, kisa tu anasubiri kubembelezwa! Jamani, tangu lini ndevu zikabembelezwa? Ni aibu iliyopitiliza dume zima kusubiri kubembelezwa kwa maneno matamu kama mtoto aliyenyimwa biskuti.

Ukweli unaouma ni kwamba: mwanamume halisi hanuni. Kununa ni ishara ya udhaifu mkubwa wa kisaikolojia na kushindwa kuhimili shinikizo la maisha. Duniani kote, changamoto ndizo zinazomfanya mwanamume aitwe mwanamume. Ukipishana na wenzako kifikra au kiuchumi, mwanaume thabiti anajipanga, anasonga mbele, na anakabiliana na hali halisi kwa ukomavu.

​Kama unahisi una tabia ya kununa kila unapoguswa, labda ni muda mwafaka wa kubadili mavazi yako. Badala ya kuvaa suruali thabiti na mikanda ya ngozi, anza kuvaa magauni labda itasaidia kuhalalisha hiyo midomo yako inayovimba kila saa. Maisha ni uwanja wa mapambano; hakuna tuzo ya mwanamume anayejua kununa vizuri zaidi.

​Acheni unyonge na tabia za kike zilizovuka mipaka. Ukikosana na mwenzako, pasua mbarika, zungumza kiume, malizeni yaishe, kisha mnywe kikombe cha kahawa pamoja.

Heshima ya mwanamume ipo kwenye kifua chake cha chuma kinachobeba mizigo ya maisha, sio kwenye midomo iliyovimba kwa usongo wa mawazo. Simama kiume, kabiliana na changamoto na uache kununa!

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Kukosana katika ndoa ni fursa kwa wenza, msinune01009-08-2026
2Komenti hasi mitandaoni zinavyogeuka shubiri kwa watumiaji09.3212-08-2026
3Ongezeko la wahitimu wa vyuo, wadau watoa pendekezo01010-08-2026
4Tumtazame mwanamke kama injini ya maendeleo08.5709-08-2026
5Yanayowasubiri wahitimu mitaani0020-07-2026
6Hivi ndivyo mwanachuo anaweza kujiajiri01012-08-2026
7Мужик все правильно сказал07.3512-08-2026
8Re: Разговоры о погоде, времена года2330-06-2026
9Kutoka 'ombaomba' hadi kumiliki bajaji2620-07-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 9. Тональность: 0. Информативность: 9.32. Источник: www.mwananchi.co.tz.