Mafanikio ya kambi ya matibabu ya moyo iliyofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) nchini Comoro yamefungua fursa ya ushirikiano mpya baada ya uongozi wa Kisiwa cha Anjouan, kuomba huduma hizo ziwe zinaendelea kutolewa kupitia makubaliano ya muda mrefu.
Dar es Salaam. Mafanikio ya kambi ya matibabu ya moyo iliyofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) nchini Comoro yamefungua fursa ya ushirikiano mpya baada ya uongozi wa Kisiwa cha Anjouan, kuomba huduma hizo ziwe zinaendelea kutolewa kupitia makubaliano ya muda mrefu.
Ombi hilo limewasilishwa leo Jumatano, Agosti 12, 2026 na Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Dk Salim Hamad, alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge, kujadili namna taasisi hiyo inavyoweza kuendeleza huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo nchini humo.
Dk Hamad amesema Comoro bado haina huduma za kibingwa za matibabu ya moyo, hali inayowalazimu wagonjwa wengi kusafiri nje ya nchi kutafuta matibabu.
Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Dk Salim Hamad (kushoto), alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge, kujadili namna taasisi hiyo inavyoweza kuendeleza huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo nchini Comoro.
Amesema mafanikio ya kambi ya matibabu iliyofanywa na JKCI katika Kisiwa cha Anjouan Oktoba mwaka jana yameongeza imani ya viongozi na wananchi wa Comoro kuhusu uwezo wa taasisi hiyo.
"Nilipokutana na uongozi wa Kisiwa cha Anjouan waliniomba niufikishe ujumbe kwa JKCI kuwa wanahitaji kuingia makubaliano ya kuendelea kufanya kambi za matibabu ya moyo. Hii ni hatua kubwa kwa nchi yetu katika kupeleka huduma za kibingwa nje ya mipaka yake," amesema Dk Hamad.
Kwa upande wake, Dk Kisenge amesema mwitikio mkubwa wa wananchi wakati wa kambi hiyo umeonyesha kuwa mahitaji ya huduma za moyo nchini Comoro ni makubwa, hivyo kuna umuhimu wa kuimarisha ushirikiano huo.
Amesema JKCI inaandaa mkakati wa kuongeza uelewa kuhusu huduma zake nchini Comoro ili wananchi wengi zaidi wafahamu fursa ya kupata uchunguzi na matibabu ya moyo kupitia taasisi hiyo.
"Tunataka wananchi wa Comoro wafahamu huduma tunazotoa ili wapate matibabu kwa urahisi zaidi badala ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma hizi nje ya nchi yao," alisema Dk Kisenge.
Hatua hiyo inatarajiwa kuimarisha ushirikiano wa sekta ya afya kati ya Tanzania na Comoro, huku JKCI ikiendelea kupanua wigo wa utoaji wa huduma za kibingwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Visiwa vya Bahari ya Hindi.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Mashindano ya Feassa yafunga shule Morogoro Mjini, ikiibua sintofahamu | 0 | 10 | 10-08-2026 |
| 2 | Mafanikio darasani yanaanzia kwenye afya ya mwili | 0 | 7.83 | 10-08-2026 |
| 3 | Около 50 пациентов поступили в больницу в Коммунарке за последние сутки | 0 | 0 | 12-04-2020 |
| 4 | Резиденты ТОР "Комсомольск" за пять лет реализовали проекты на 2,2 млрд рублей | 0 | 0 | 25-06-2020 |
| 5 | Muhimbili yatenganisha pacha walioungana | 0 | 7.23 | 10-08-2026 |
| 6 | В медучреждения Москвы закупили 25 новых аппаратов ЭКМО | 0 | 0 | 30-08-2021 |
| 7 | Usalama wa kihisia msingi muhimu utekelezaji wa mtalaa | 0 | 5.56 | 10-08-2026 |
| 8 | Еще около 90 пациентов поступили на лечение в больницу в Коммунарке | 0 | 0 | 26-04-2020 |
| 9 | АСИ наградило компании с лучшими инклюзивными практиками | 0 | 0 | 25-11-2025 |
| 10 | Станция скорой помощи в Москве получила 60 систем сердечно-легочной реанимации | 0 | 0 | 29-01-2021 |