Siku chache baada ya kutoka Msumbiji, mfanyabiashara na rais wa MeTL Group, Mohammed Dewji, maarufu Mo ameanza kuangalia fursa mpya za uwekezaji nchini Botswana ikiwa ni katika hatua za kuendelea kutanua shughuli zake za biashara.
Alhamisi, Agosti 27, 2026

Rais wa Botswana, Duma Boko, (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Mohammed Dewji kuhusu uwekezaji nchini Botswana.
Dar es Salaam. Siku chache baada ya kutoka Msumbiji, mfanyabiashara na rais wa MeTL Group, Mohammed Dewji, maarufu Mo ameanza kuangalia fursa mpya za uwekezaji nchini Botswana ikiwa ni katika hatua za kuendelea kutanua shughuli zake za biashara.
Dewji amesaka fursa hizo baada ya kushiriki mikutano ya ngazi ya juu iliyojikita katika mabadiliko ya uchumi wa nchi hiyo, mazingira ya uwekezaji na ukuaji wa sekta binafsi.
Katika ziara yake jijini Gaborone, Dewji alikutana na Rais wa Botswana, Duma Boko, Makamu wa Rais, Ndaba Gaolathe, Gavana wa Benki Kuu ya Botswana pamoja na viongozi wa Botswana Stock Exchange.
Mikutano hiyo imefanyika wakati serikali ya Rais Boko ikiendeleza Programu ya mageuzi ya kiuchumi ya Botswana (BETP) ambao unalenga kupanua vyanzo vya uchumi zaidi ya utegemezi wa almasi, kuvutia uwekezaji mpya na kujenga maeneo mapya ya ukuaji.
Mazungumzo hayo yaligusa fursa za kuongeza ushiriki wa sekta binafsi pamoja na maeneo ambayo MeTL Group ina nia ya kuyachunguza zaidi yakiwemo nishati jadidifu na huduma za kifedha.

Rais wa Botswana, Duma Boko, (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Mohammed Dewji kuhusu uwekezaji nchini Botswana.
Dewji amesema mikutano hiyo imempa picha nzuri zaidi ya mwelekeo wa uchumi wa Botswana na dhamira ya nchi hiyo kutumia uwekezaji kama kichocheo cha ukuaji.
“Botswana imejenga msingi imara. Kilichonivutia ni umakini ambao nchi inaweka katika hatua yake inayofuata ya ukuaji. Kuna msisitizo wa kuvutia uwekezaji, kujenga viwanda vinavyoweza kushindana na kuweka mazingira ambayo sekta binafsi inaweza kustawi,” amesema.
Dewji ameyasema hayo wakati ambao MeTL Group imejenga shughuli mbalimbali za biashara barani Afrika katika sekta za viwanda, kilimo, nishati, usafirishaji na maeneo mengine.
Amesema wakati MeTL Group ikiendelea kupanua uwepo wake kikanda, Botswana ni miongoni mwa masoko yenye fursa za uwekezaji na ushirikiano wa muda mrefu.
“MeTL tunapoendelea kukua Afrika, tunaangalia masoko ambayo tunaweza kupeleka mitaji, uzoefu na dhamira ya kujenga kwa muda mrefu. Tunaona fursa nzuri Botswana na tunatarajia kuendelea kuchunguza maeneo ambayo tunaweza kuwekeza na kujenga thamani pamoja,” amesema.

Rais wa Botswana, Duma Boko, (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Mohammed Dewji katika mazungumzo kuhusu uwekezaji nchini Botswana.
Ziara hiyo pia imeonyesha nafasi iliyopo ya kuimarisha zaidi uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Botswana, wakati biashara za Kiafrika zikizidi kutafuta uwekezaji, ushirikiano na masoko mapya ndani ya bara.
Dewji ametoa shukurani kwa Neo Mooki, Mwenyekiti wa Botswana Stock Exchange, kwa mchango wake katika kuratibu na kufanikisha mikutano hiyo, pamoja na timu yake, Oupa na Thapelo, kwa mapokezi na ushirikiano walioutoa wakati wa ziara hiyo.
Ziara ya Dewji Botswana imekuja ikiwa ni siku chache tangu alipotoka nchini Msumbiji ambapo aliahidi kuwekeza zaidi ya Sh661.93 bilioni.
Analolifanya sasa ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan la kuwataka wafanyabiashara wa Tanzania kuendelea kusaka fursa za uwekezaji nchi jirani.
Aliyasema hayo alipokuwa akifanya kikao na wadau wa Sekta binafsi ikiwa ni hatua za mwanzoni kuelekea utekelezaji wa Dira 2050 inayolenga kukuza pato la Taifa hadi kufikia dola 1 trilioni za Marekani.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Bwawa la Nyerere kufungua zaidi fursa kuvutia uwekezaji | 0 | 6.49 | 27-08-2026 |
| 2 | Namibia: Namibian, Chinese Firms Sign Clean Energy Joint Venture | 0 | 11.43 | 10-07-2026 |
| 3 | Namibia: Chinese Investors Urged to Explore Investment Opportunities in Namibia | 0 | 10.38 | 09-07-2026 |
| 4 | Президент Мозамбика сообщил о планируемых реформах в стране, заявил Лавров | 0 | 5 | 09-07-2026 |
| 5 | Mozambique: Mozambique and China Should Take Their Economic Ties to Higher Level - Cta | 0 | 6.35 | 23-07-2026 |
| 6 | Президент Уганды пригласил российские компании к сотрудничеству в фармацевтике | 0 | 0 | 27-07-2023 |
| 7 | Президент Мозамбика намерен обсудить с Путиным привлечение инвестиций | 0 | 0 | 21-08-2019 |
| 8 | Президент Мозамбика призвал повысить уровень экономического сотрудничества с Россией | 0 | 0 | 21-08-2019 |
| 9 | Лавров подвёл итоги визита в Мозамбик | 0 | 5 | 09-07-2026 |