Kwa miaka mingi, fedha taslimu zimekuwa kiini cha miamala ya kila siku visiwani Zanzibar. Kuanzia kulipia nauli ya basi na kununua chakula katika duka la mtaani hadi kulipa bili na kutuma fedha kwa familia, noti na sarafu zimeendelea kuwa sehemu inayofahamika ya maisha ya kila siku.
Alhamisi, Agosti 27, 2026

Kwa miaka mingi, fedha taslimu zimekuwa kiini cha miamala ya kila siku visiwani Zanzibar. Kuanzia kulipia nauli ya basi na kununua chakula katika duka la mtaani hadi kulipa bili na kutuma fedha kwa familia, noti na sarafu zimeendelea kuwa sehemu inayofahamika ya maisha ya kila siku.
Hata hivyo mambo yanabadilika kwa kasi hivi sasa, baadhi ya miamala hiyo inahama kutoka katika matumizi ya fedha taslimu kwenda kwenye simu za mkononi, pochi za kidijitali na kadi janja, hali inayofanya malipo yasiyotumia fedha taslimu kuwa sehemu ya karibu zaidi ya maisha ya kila siku ya watumiaji wa kawaida.
Moja ya mifano iliyo wazi zaidi sasa inaonekana katika barabara za Zanzibar, ambako huduma mpya ya mabasi ya umeme imekuja na uzoefu wa malipo unaotofautiana kwa kiasi kikubwa na safari za kawaida za daladala.
Badala ya kumpa kondakta fedha taslimu, abiria wanaotumia mabasi ya umeme ya ZanBus hulipa kupitia kadi janja zilizounganishwa na mfumo wa malipo wa kidijitali wa Mixx by Yas. Abiria anapanda, anagusa au kuwasilisha kadi, nauli inakatwa na safari inaendelea.
Ni muamala rahisi, lakini nyuma ya mguso huo kuna mabadiliko mapana zaidi katika namna watu wanavyolipa, namna waendeshaji wa usafiri wanavyokusanya mapato na jinsi huduma za kifedha za kidijitali zinavyozidi kuingizwa katika shughuli za kiuchumi za kila siku.
Kwa hiyo, mfumo huo mpya hauhusu tu kubadilisha aina moja ya usafiri kwenda nyingine. Pia unakuwa jaribio la kweli la kuona jinsi watumiaji wanavyoweza kuzoea kwa haraka namna ya kulipia huduma muhimu ya kila siku bila kutumia fedha taslimu.
Mabasi ya umeme yalianza shughuli za kibiashara Agosti 1, 2026, baada ya kuzinduliwa kwa kundi la kwanza la mabasi 15. Mradi mpana wa usafiri wa umma unatarajiwa kupanuka kwa kiasi kikubwa, hivyo kufanya mfumo wa malipo kuwa sehemu muhimu ya ajenda pana ya Zanzibar ya mageuzi ya usafiri na kidijitali.
Njia za awali za mabasi ya umeme ni Malindi–Buyu na Malindi–Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, ambapo kila safari kwa abiria wa kawaida ni Sh700 huku wanafunzi na wazee wenye umri wa miaka 70 na zaidi wakilipa Sh350, sawa na nusu ya nauli ya kawaida.
Namna kulipia safari za mabasi ya umeme
Pamoja na changamoto ambazo zimeibuka mpaka sasa, kwa abiria waliozoea kupanda daladala wakiwa na fedha taslimu mkononi, mabadiliko hayo yanahitaji kubadilika kwa mazoea, kwani hivi sasa huna sababu ya kubeba pesa taslimu tena.
“Watu wanaanza kuuzoea taratibu. Siku ya kwanza ilikuwa changamoto kwa sababu kulikuwa na abiria wengi na wengi wao hawakujua namna ya kutumia mfumo huo au mahali pa kupata kadi. Lakini kadiri muda unavyokwenda, abiria wanajifunza kutoka kwa wenzao, huku mimi na madereva wa mabasi tukiwaongoza,” alisema kondakta wa basi la umeme, Rajab Mohammed.
Ingawa teknolojia ya malipo yasiyotumia fedha taslimu tayari ipo, watumiaji bado wanajifunza namna ya kuiingiza katika maisha yao ya kila siku.
Kwa msafiri, kutolazimika kutafuta chenji sahihi kunaweza kuonekana kama urahisi mdogo. Lakini urahisi huo unapojirudia katika mamia au maelfu ya safari, unaweza taratibu kuathiri tabia za watumiaji.
Kwa upande mwingine, mfumo wa malipo ya kidijitali unaweza kutengeneza kumbukumbu ya kielektroniki ya miamala. Hilo linaweza kuwapa waendeshaji wa usafiri uelewa mzuri zaidi wa fedha zilizokusanywa na kusaidia katika upatanishaji wa mapato na utoaji wa taarifa.
Kwa mzazi ambaye watoto wake hutumia usafiri wa umma mara kwa mara, mfumo usiotumia fedha taslimu unaweza kupunguza hitaji la kuandaa fedha za matumizi kwa kila safari na badala yake akaweka fedha katika kadi yake ambayo anajua itamfaa kwa siku kadhaa.
Meneja wa Biashara Mixx, Kanda ya Zanzibar Salum Nassor Mohamed anasema tangu kuanza kwa huduma ya ZanBus, Mixx by Yas imekuwa mtoa huduma wa kipekee wa malipo kwa mfumo wa tiketi ambapo zaidi ya abiria 5,000 wanahudumiwa kila siku.
“Kadri idadi ya mabasi inavyoongezeka, matumizi ya malipo ya kidijitali yanatarajiwa kukua kwa kasi zaidi. Lengo la mradi ni kufikia takribani mabasi 500 yatakayotoa huduma kwa Mkoa mzima wa Mjini Magharibi,” anasema Mohamed.
Anasema Mixx by Yas inajivunia kushirikiana na Serikali, taasisi na sekta binafsi kuwezesha malipo ya kidijitali katika huduma mbalimbali zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
“Ushiriki wa Mixx katika ZanBus umeufanya mradi huo wa kisasa wa kidijitali pekee, hakuna matumizi ya pesa Taslim. Halii imeongeza zaidi matumizi ya malipo ya kidijitali kwa Zanzibar, ambapo abiria wanaweza kununua na kuweka salio kwenye kadi zao za usafiri kupitia Mixx,” anasema.
Mohamed anasema mbali na malipo kwa usafiri wa mabasi pia wanawezesha ulipaji wa maegesho ya vyombo vya moto katika Mamlaka ya Mji Mkongwe, malipo ya wakulima wa karafuu kupitia Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC), pamoja na malipo ya faini za makosa ya barabarani kupitia KWASILVA kwa kushirikiana na ZARTSA.
“Katika eneo la huduma za kifedha na ujumuishi wa kifedha, Mixx pia imewezesha huduma ya akiba ya Kikoba kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Ushirika, SOS Children’s Villages, Zanzibar Maisha Bora Foundation, pamoja na taasisi mbalimbali za asasi za kiraia na kijamii,” anasema.
Hali ilivyo kwa biashara nyingine
Visiwani hapa, mabadiliko kuelekea malipo yasiyotumia fedha taslimu yanaenea pia nje ya usafiri wa umma. Kwa wafanyabiashara wadogo, migahawa, maduka na watoa huduma wengine, kukubali malipo ya kidijitali kunaweza kutoa njia mbadala ya kushughulika na fedha taslimu siku nzima.
Mteja anaweza kulipa kielektroniki huku biashara ikipokea kumbukumbu ya muamala. Kwa biashara zinazofanya miamala mingi midogo, kumbukumbu hizo zinaweza kurahisisha kufuatilia mauzo, kulinganisha mapato na kuelewa kiasi cha fedha kilichopita katika biashara. “Kwa biashara ndogo, kujua kiasi ulichopokea na kuweza kuona miamala kunaweza kusaidia katika uwajibikaji. Pia kunampa mwenye biashara uelewa mkubwa zaidi wa fedha zinazoingia katika biashara,” alisema Bi Idd.
Mtalii anayelipa kielektroniki katika hoteli, msafiri anayetumia kadi janja kupanda basi na mfanyabiashara mdogo anayepokea malipo kwa simu vinaweza kuonekana kuwa miamala tofauti.
Mohammed anasema kupitia kupitia mtandao wetu wa mawakala ulioenea visiwani wakiwa na zaidi ya mawakala elfu 20 Mixx by Yas inaendelea kuongeza ujumuishi wa huduma za kifedha Zanzibar kwa kuwapa wananchi njia rahisi, salama na nafuu ya kufanya malipo na kupata huduma za kifedha kupitia simu zao.
“Tunaona Zanzibar ikiingia kwenye uchumi wa kidijitali kwa kasi zaidi katika miaka 5 mpaka 10 ijayo. Malipo kwa njia ya simu yataendelea kuhamia kutoka kuwa njia mbadala na kuwa sehemu ya msingi ya maisha ya kila siku kuanzia usafiri, biashara, huduma za Serikali, utalii, afya, elimu hadi huduma za kifedha,” anasema.
Aidha Mahammed alisema Mixx, inaamini kuwa mustakabali huo utajengwa kupitia mifumo inayounganisha wananchi, wafanyabiashara, taasisi za Serikali na sekta binafsi katika mfumo mmoja wa malipo wa kidijitali.
“Lengo si kuwezesha malipo pekee, bali kujenga mazingira ambayo kila mwananchi na biashara, hata wale ambao hawajafikiwa kikamilifu na huduma za benki. Zanzibar ina fursa kubwa ya kuwa mfano wa matumizi ya malipo ya kidijitali katika huduma za umma na sekta binafsi, na Mixx by Yas itaendelea kuwa sehemu muhimu ya safari hiyo,” anasema.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Tanzania yaanza kupigania chakula chake kitambulike kimataifa | 0 | 5 | 20-07-2026 |
| 2 | Waliopata ajira mtandaoni kupatiwa mikopo | 0 | 9.33 | 27-08-2026 |
| 3 | Ukweli kuhusu maziwa kwenye matibabu | 0 | 6.66 | 28-08-2026 |
| 4 | Stanbic benki yarahisisha malipo ya Shilingi China | 0 | 5.72 | 28-08-2026 |
| 5 | MBEGU YA UCHUMI: Kugeuza umeme wa ziada kuwa fursa ya kiuchumi | 0 | 7.3 | 27-08-2026 |
| 6 | Wakati sahihi wa kununua hisa ni huu | 0 | 6.46 | 27-08-2026 |
| 7 | Afya bora uzeeni inaanzia kwenye ujana | 0 | 6.82 | 28-08-2026 |
| 8 | Tiba asili si uchawi, wananchi waelimishwa | 0 | 6.66 | 27-08-2026 |
| 9 | Songwe waanza mpango wa kutokomeza utoro shuleni | 0 | 4.68 | 27-08-2026 |
| 10 | Safari ya mwonjaji wa taifa hadi kukutana na Wema Sepetu | 0 | 7.54 | 27-08-2026 |